Aidha, katika utambulisho huo, Dkt. Mwasse amewafahamisha kwamba Mha. Shamika amechukua nafasi ya Bw. Ali aliyekuwa Kamishina Msaidizi wa Uchimbaji kutoka Wizara ya Madini, akisema mabadiliko haya ni ya kawaida katika utumishi wa umma.
Katika salamu zake kwa wafanyakazi, Bw. Ali ameomba kila mfanyakazi kutimiza majukumu yake kwa kujituma, kufanya kazi kwa pamoja, kupendana, kufanya kazi kwa uadilifu na kuridhika kwa kile mtu anachokipata na kushirikiana pamoja kwenye kazi.
Meneja Mkuu aliyemaliza muda wake Mha. Shamika ametoa shukrani kwa wafanyakazi wote wa STAMIGOLD kwa ushirikiano waliompatia na ameomba Meneja Mkuu mpya kupewa ushirikiano zaidi kwani alishawahi fanya nae kazi tangu mwaka 2006 na anafanya kazi vizuri. Mha. Shamika amemuhakikishia Bw. Ali ushirikiano katika kukamilisha majukumu aliyokuwa nayo kama kuhakikisha mgodi unaunganishwa katika gridi ya umeme ya Taifa ambayo inasimamiwa na TANESCO.
Wafanyakazi wa STAMIGOLD wametoa shukrani kwa Mha. Shamika kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kuendeleza mgodi, kuthamini michango ya wafanyakazi katika uzalishaji na kupendekeza Bw. Ali aangalie sana masilahi ya wafanyakazi, kuboresha uzalishaji pamoja na kusikiliza maoni mbali mbali ya wafanyakazi.