TANESCO Kuokoa Mabilioni ya Serikali STAMIGOLD

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Dkt. Alexander Kyaruzi amesema kuwa TANESCO inajipanga kufikisha Umeme wa Gridi ya Taifa katika Mgodi wa STAMIGOLD Biharamulo ili kuokoa kiasi cha Takribani Shilingi bilioni 8.4 zinazotumika kwa mwaka katika mgodi huo kuzalisha umeme ghali wa mafuta mazito ya dizeli kwaajili kuendesha mitambo ya Mgodi huo.

“Baada ya bodi kutembelea mgodi na kujionea mahitaji ya mgodi na hasara wanayoipata kutokana na kukosa huduma ya umeme nafuu wa TANESCO,tutashirikiana na Menejimenti kufikisha umeme katika mgodi huu mapema iwezekanavyo kutokea Mkoani Geita umbali wa kilomita 90 mara baada ya kukamilika kwa mradi wa Bulyahnulu Geita mwezi juni 2020” Alisema Dkt.Kyaruzi.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa mgodi wa STAMIGOLD, Mhandisi Gilay Shamika amesema kuwa, kutokana na kukosa umeme nafuu wa TANESCO, gharama za kiuendeshaji ni kubwa lakini endapo mgodi utaunganishwa na umeme wa TANESCO, itasaidia kukua kwa mgodi na kuongeza mapato pamoja na mchango wa mgodi Serikalini.
“Hivi sasa tunatumia takribani Shilingi bilioni 1 kuzalisha umeme kwa mwezi lakini kama tukiunganisha umeme wa TANESCO tutalipia takriban shilingi milioni 300 kwa mwezi hivyo tutaokoa takriban bilioni 8.4 ambazo zitaingia kwenye mapato ya Mgodi na Serikali” Alisema Mhandisi Shamika.

Connect with us

Stamigold Company Limited, Plot # 417/418, United Nations Road, Upanga, Dar es salaam

  • +255 (22) 2151717/3
  • info@stamigold.co.tz

 

Newsletter

Enter your email address

Search