Kaimu mkurugenzi mkuu mpya wa Shirika la Madini la Taifa-STAMICO

KAIMU MKURUGENZI MKUU STAMICO AFANYA ZIARA STAMIGOLD

Kaimu mkurugenzi mkuu mpya wa Shirika la Madini la Taifa-STAMICO Kanali Sylivester Damian Ghuliku alifika mgodini hapo siku ya tarehe 16 Machi mwaka huu akiwa ameongozana na Bi. Zena Kongoi ambaye ni kaimu mkurugenzi Uchimbaji na huduma za kihandisi STAMICO. Hii ikiwa ni ziara yake ya kwanza kufika Stamigold toka ateuliwe kushika nyadhifa hiyo siku za hivi karibuni.  

Katika ziara yake iliyodumu kwa takribani siku mbili (16 hadi 17 Machi 2018), Mkurugenzi huyo alipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya mgodi ikiwemo; Uchenjuaji, uchimbaji/Pit na katika mabwawa ya visusu (TSF) ambako aliweza kusikiliza maelezo ya kitaalamu kutoka kwa wataalamu husika.

 Kanali Sylivester Ghuliku alifanya mazungumzo na menejimenti na kupata taarifa fupi ya maendeleo na mikakati ya mgodi, naye akawa na haya ya kuzungumza;

Menejimenti inajukumu la kuhakikisha kampuni inaonyesha mwanga kwa kufanya kazi kwa bidii,weledi,kujiamini,uaminifu na uzalendo wa hali ya juu ili kufuta makosa ya hapo awali na kurudisha dhana ya uaminifu kwa serikali. Elimu na uzoefu uzingatiwe katika utendaji,wataalamu watumie vema taaluma zao katika kuiletea tija kampuni na Taifa kwa ujumla,hatua zinazofaa zichukuliwe haraka kukarabati mitambo na mashine aliongeza Mkurugenzi huyo.

Aidha Menejimenti ihakikishe inafanya utafiti/upembuzi yakinifu kwa taarifa za kijiolojia na miradi yote ili kuwa na uhakika na taarifa hizo ili kuiwezesha kampuni iwekeze katika miradi yenye tija na faida. Mmeonyesha nia na serikali iko tayari kuunga mkono juhudi zenu kwa kuonyesha watanzania tunaweza aliongeza Mkurugenzi huyo.

Baada ya maelezo na maelekezo hayo ya Kaimu Mkurugenzi mkuu STAMICO, kaimu meneja mkuu wa mgodi wa Stamigold Dr. Venance B. Mwasse alipata fursa ya kuzungumza machache kwa niaba ya Menejimenti akionyesha furaha na matumaini ya ushirikiano wa STAMICO/serikali na kampuni ya Stamigold, alianza kwa kumshukuru Kanali Ghuliku kwa kutumia muda wake hadhimu kwa kutembelea Mgodini hapo na kupata wasaha wa kusikiliza changamoto zinazoukabili mgodi na kuonyesha nia ya kuboresha ushirikiano na kuahidi kushiriki kikamilifu ili kuhakikisha Mgodi unaendelea.

Dr. Venance B. Mwasse alitumia nafasi ile kumpongeza kanali Sylivester kwa kuteuliwa kwake kuwa kaimu Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Madini na kumhakikishia ushirikiano wa hali na mali. Alisisitiza kuwa; Menejimenti ya Stamigold inaahidi kufanyia kazi maelekezo yote, utafiti utafanyika,menejimenti itasimamia misingi ya nidhamu na uadilifu katika kazi,Elimu,ubunifu na uzoefu utazingatiwa katika utekelezaji wa majukumu ya kila mmoja, na kuhakikisha kila mfanyakazi anatekeleza wajibu wake kwa manufaa ya kampuni na Taifa kwa ujumla aliongea kaimu Meneja huyo.   

Nae Mrakibu Jiolojia Yusuph Mbagga alikuwa na haya ya kusema; kitengo cha jiolojia kinaendelea kufanya utafiti mdogo na kutokana na utafiti huo hadi sasa Mgodi una zaidi ya mashapo 537,271 yenye wakia 21,765 zenye thamani ya wastani wa 1.26.

Hata hivyo Idara na Menejimenti kwa ujumla ikishirikiana na kaimu meneja mkuu inaahidi kuendelea kuibua miradi mingi zaidi ili kuongeza muda wa maisha ya mgodi na kujenga imani kubwa kwa serikali kuwa Stamigold ya Watanzania inaweza alisisitiza Yusuph Mbagga.

 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu STAMICO                                             

Kaimu mkurugenzi mkuu mpya wa Shirika la Madini la Taifa-STAMICO Kanali Sylivester Damian Ghuliku...        

Read More

 

Ag. Director General Visit

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji STAMICO Mhandisi Hamis Komba, siku za hivi karibuni alifanikiwa kufanya ziara ya kikazi katika Mgodi wa STAMIGOLD 

Read More

Ag. Director General Visit

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji STAMICO Mhandisi Hamis Komba, siku za hivi karibuni alifanikiwa kufanya ziara ya kikazi katika Mgodi wa STAMIGOLD 

Read More

Ag. Director General Visit

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji STAMICO Mhandisi Hamis Komba, siku za hivi karibuni alifanikiwa kufanya ziara ya kikazi katika Mgodi wa STAMIGOLD 

Read More

Ag. Director General Visit

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji STAMICO Mhandisi Hamis Komba, siku za hivi karibuni alifanikiwa kufanya ziara ya kikazi katika Mgodi wa STAMIGOLD 

Read More

Corperate Info

STAMIGOLD Company Limited was incorporated on 28th October, 2013. The Company is a subsidiary of the State...

Read More

About us       Terms of use       Privacy policy       contact us                                                                                                                                                                                                                   Designed by Microtelecomms

JoomShaper